#Local News

JUNET: ODM HAITABAKI UPINZANI MILELE

Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed amesema chama cha ODM bado kinasimamia misingi na maadili kilichoasisiwa nayo, licha ya kuwa sehemu ya mpangilio wa serikali ya ushirikiano mpana.

Junet amesema baadhi ya watu wanapinga ushirikiano huo kwa sababu hawataki ODM iwe serikalini, akisema hakuna sheria inayolazimisha chama hicho kubaki katika upinzani milele.

Amesema ODM iko tayari kuunda serikali na viongozi wenye mawazo yanayofanana, ambao wataheshimu misingi na maadili ya chama hicho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *