VIONGOZI WA ODM WAUNGA MKONO AJENDA YA BEYOND VISION 2030
Msimamo kuhusu ajenda mpya ya maendeleo ya taifa unaendelea kujitokeza kutoka kwa viongozi wa kisiasa, huku baadhi ya vyama vikieleza kuunga kwa mkakati huo wa baada ya Dira ya 2030.
Viongozi wa ODM wakiongozwa na Oburu Odinga wameunga mkono ajenda ya Beyond Vision 2030, wakisema itasaidia kuimarisha maendeleo na usawa nchini.
Viongozi hao wamesema wanaunga mkono ajenda hiyo kwa kuwa chama hicho kilishiriki katika kuasisi Dira ya 2030, huku wakiwakosoa viongozi wa upinzani kwa kile wanachodai ni siasa zisizo na dira ya maendeleo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































