MOTO WATEKETEZA MAJENGO KANGEMI
Moto umezuka katika majengo ya makazi katika eneo la Posta, Kangemi jijini Nairobi, huku watu kadhaa wakihofiwa kunaswa ndani ya majengo hayo.
Timu ya kuzima moto ya Serikali ya Kaunti ya Nairobi inaendelea na juhudi za kudhibiti moto huo, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijabainika na idadi ya watu walionaswa au kujeruhiwa ikiwa bado haijafahamika.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































