#Rugby #Sports

UPPER HILL NA BOKOLI WATINGA ROBO FAINALI YA RAGA YA WACHEZAJI SABA

Shule za Upper HillBokoli na Itigo Girls zimefuzu kwa hatua ya robo fainali ya raga ya wachezaji saba katika Michezo ya Kitaifa ya Muhula wa Pili ya shule za upili inayoendelea katika Chuo cha M-Pesa Foundation Academy, Thika.

Upper Hill ilianza kampeni yake kwa ushindi wa alama 7-0 dhidi ya All Saints Embu kabla ya kuibwaga Friends School Anjego kwa alama 19-14, huku Bokoli ikiifunga Friends School Anjego kwa alama 21-5 na baadaye kuichapa All Saints Embu kwa alama 28-5 na kufuzu katika hatua ya timu nane bora.

Kocha wa Upper Hill, Eustace Sifuna, amesema ushindani ni mkali lakini ana imani kikosi chake kina uwezo wa kutwaa ubingwa Naye kocha wa Bokoli, Eliud Okwemba, akipongeza wachezaji wake kwa kufuzu robo fainali katika ushiriki wao wa kwanza kwenye mashindano hayo ya kitaifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *