MAHAKAMA YAIAGIZA SERIKALI KUWAPA FIDIA WAATHIRIWA WA UTEKAJI NYARA
Serikali imeagizwa kutenga shilingi milioni 105 kutoka kwa mfuko wa fidia ili kuwalipa waathiriwa wa mateso, kutoweshwa kwa lazima na utekaji nyara, agizo hilo limetolewa na Jaji Gregory Mutai huku kesi inayopinga mchakato wa uthibitishaji wa waathiriwa ikiendelea mahakamani.
Jaji Mutai ametoa agizo hilo kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi linalopinga mchakato wa uthibitishaji ulioanzishwa na serikali kwa ajili ya kuwabaini waathiriwa wanaostahili fidia, kufuatia Tangazo la Rais nambari moja la mwaka 2026.
Mahakama pia imetoa amri ya muda inayowazuia walalamikiwa wa kwanza na wa pili kutekeleza, kutumia au kuchukua hatua yoyote kwa kuzingatia mchakato huo wa uthibitishaji unaopingwa, hadi ombi hilo litakaposikilizwa na kuamuliwa.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































