KINDIKI AELEZA UMUHIMU WA TAIFA KUWA NA UONGOZI DHABITI
Naibu Rais Kithure Kindiki amesema Kenya ina uwezo wa kujiunga na mataifa tajiri na yaliyoendelea iwapo nchi itaendelea kuwa na uongozi thabiti, kujenga imani katika uwezo wake na kulinda sera za maendeleo ya muda mrefu dhidi ya kuvurugwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mjadala wa kitaifa kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Baada ya 2030 Kindiki amesema Kenya inapaswa kutumia ajenda hiyo mpya ya maendeleo ya muda mrefu kuamua namna ya kuipeleka nchi katika kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kindiki aidha amesema Kenya tayari imeweka msingi unaoweza kuiwezesha kubadilika na kuwa taifa tajiri, akisisitiza umuhimu wa kudumisha uongozi na sera zinazolenga maendeleo ya muda mrefu.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































