#Local News

DPP AONYA KUHUSU MAUDHUI HATARI MTANDAONI

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ameonya kuhusu ongezeko la maudhui hatari kwenye majukwaa ya kidijitali, akisema yanahatarisha maadili na maendeleo ya watoto.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Ingonga amesema watoto wanaendelea kuwa miongoni mwa watumiaji walio katika hatari zaidi ya kuathiriwa na maudhui yasiyofaa mtandaoni, akitaka hatua za pamoja kuchukuliwa ili kuwalinda.

Akizungumza Bungoma, Ingonga ametoa wito kwa familia, shule, taasisi za kidini na mashirika ya serikali kushirikiana kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya maudhui yanayoweza kuathiri mwenendo na maendeleo yao ya kijamii.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

DPP AONYA KUHUSU MAUDHUI HATARI MTANDAONI

WAUGUZI WAKATAA KUSITISHA MGOMO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *