#Local News

TAHARUKI HOMA BAY KABLA YA MKUTANO WA LINDA MWANANCHI

Mvutano wa kisiasa unaongezeka Homa Bay kuelekea mkutano wa Linda Mwananchi unaotarajiwa kufanyika Jumapili, huku viongozi wa vuguvugu hilo wakidai kuna mipango ya kutumia magenge yenye silaha kuvuruga mkutano huo.

Viongozi hao wamesema tayari wamemjulisha Mkuu wa Polisi Douglas Kanja kuhusu madai hayo na wamemtaka kuhakikisha usalama wa washiriki kabla na wakati wa mkutano.

Licha ya hofu hiyo, viongozi wa Linda Mwananchi wamesisitiza kuwa mkutano utafanyika kama ulivyopangwa, huku wakiitaka serikali kuhakikisha amani na usalama wa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *