METHU: WANANCHI WAKO TAYARI KULINDA KURA ZAO
Seneta wa Nyandurua John Methu amesema wananchi wameonyesha utayari wa kulinda kura zao wenyewe wakati wa uchaguzi, akirejelea matukio ya Ol Kalou.
Methu amesema hakuna watu waliokuwa wameajiriwa maalumu kulinda kura katika eneo hilo, bali wananchi wenyewe walihakikisha kura zao zinalindwa.
Amesema hatua hiyo inaonyesha kuwa wananchi wako tayari kushiriki kikamilifu katika kulinda haki yao ya kupiga kura.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































