RUTHU KULUNDU ATEULIWA KAMA KAIMU KATIBU WA IEBC
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC imemteua Ruth Kulundu kuwa Kaimu Katibu wa Tume na Afisa Mkuu Mtendaji.
Uteuzi huo unaanza kutekelezwa leo, Agosti 5, 2026, baada ya kumalizika kwa muda wa miezi sita wa Moses Ledama Sunkuli aliyekuwa akikaimu wadhifa huo.
Mwenye kiti wa IEBC Erustus Ethekon amesema Kulundu ataendelea kuwa kaimu katibu wa tume hiyo hadi mchakato wa kuajiri na kumteua Katibu wa Tume na Afisa Mkuu Mtendaji wa kudumu utakapokamilika.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































