#Local News

NYONG’O: DIRA YA 2060 SI MRADI WA KISIASA

Mjadala kuhusu mkakati mpya wa maendeleo ya taifa unaendelea kupamba moto huku baadhi ya viongozi wakisisitiza kuwa ajenda hiyo inapaswa kutazamwa kama mpango wa kitaifa badala ya kisiasa.

Gavana wa Kisumu Profesa Anyang’ Nyong’o amesema Dira ya 2060 si mradi wa kampeni za kisiasa bali ni mpango wa kitaifa unaolenga kuiongoza Kenya baada ya kukamilika kwa Dira ya 2030.

Nyong’o amesema Dira ya 2030 na Dira ya 2060 zinahudumia nyakati na mahitaji tofauti ya maendeleo, akibainisha kuwa Dira ya 2030 iliandaliwa kama mkakati wa kuboresha maisha ya Wakenya na imeendelea kuwa ajenda ya kitaifa badala ya  kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *