#Local News

RAIS RUTO AZINDUA RASMI KONGAMANO HUKO NAIVASHA

Rais William Ruto amesifu chama cha ODM kwa kufanya kipaumbele maslahi ya taifa hili akisema chama hicho kilifanya uamuzi muhimu wakati kenya ilikua katika njia panda

Akizungumza mjini Naivasha kaunti ya Nakuru kwenye kongamano la wabunge wa kenya kwanza na ODM Rais Ruto amesema chini ya uongozi wa aliyekuwa kiongozi wake hayati Raila Odinga na sasa Oburu Odinga chama hicho kitakumbukwa kwa  kuchagua mustakabali wa taifa hili badala ya siasa.

Rais amesema ushirikiano kati ya ODM na Kenya Kwanza umewezesha serikali kuunganisha baadhi ya sera za Azimio na mipango ya maendeleo ya kenya kwanza .

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *