#Local News

WASHUKIWA WATATU WAKAMATWA KWA MAUAJI YA NATHAN WASAMA

Maafisa wa upelelezi wanaochunguza mauaji ya mfanyabiashara Nathan Masai Wasama mwenye umri wa miaka 61 huko Cheptais, Bungoma, wamewakamata washukiwa watatu.

Wasama alipigwa risasi usiku wa Agosti 8, 2026, katika duka lake kwenye kituo cha biashara cha Tuikut, baada ya wanaume wanne kufika eneo hilo wakiwa kwenye pikipiki mbili.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mmoja wa abiria alishuka, akaingia dukani na kumpiga Wasama risasi kabla ya kutoroka na wenzake. Sababu ya mauaji hayo bado haijabainika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *