KIPRONO AELEKEZEA MACHO OLIMPIKI YA LOS ANGELES 2028
Mwanariadha chipukizi wa Kenya Emmanuel Kiprono ameweka wazi azma yake ya kushiriki Michezo ya Olimpiki ya 2028 mjini Los Angeles, baada ya kutwaa dhahabu katika mbio za mita 3,000 kwenye Mashindano ya Dunia ya Riadha ya Vijana chini ya miaka 20 huko Eugene, Marekani.
Kiprono alivunja rekodi ya mashindano hayo kwa muda wa dakika 7:28.28, akiboresha rekodi ya awali ya dakika 7:42.09 iliyowekwa na Methiopia Tadese Worku mwaka 2021 jijini Nairobi.
Baada ya ushindi huo, Kiprono amesema ataanza maandalizi mapema kwa mazoezi makali akilenga kufuzu na kuiwakilisha Kenya katika Olimpiki ya Los Angeles 2028.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































