RUTO KUKUTANA NA WAKENYA 5,000 KUJADILI RUWAZA 2060
Rais William Ruto leo anatarajiwa kukutana na zaidi ya Wakenya 5,000 kutoka kaunti zote 47 katika ukumbi KICC kwa mazungumzo ya kitaifa kuhusu mpango wa Ruwaza ya Kenya 2060.
Mazungumzo hayo yataashiria kuanza rasmi kwa ushirikishwaji wa umma huku wananchi wakitarajiwa kutoa maoni kuhusu vipaumbele vya maendeleo ya muda mrefu.
Mapendekezo yatakayowasilishwa na washiriki hao yanatarajiwa kuwa msingi wa Mkataba wa Kitaifa wa Maendeleo, ambao baadaye utabadilishwa kuwa Mswada na kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuzingatiwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































