MAANDAMANO KENYA YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 29
Kenya ilishuhudia maandamano 453 katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 29 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2025.
Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International, ongezeko hilo limechangiwa zaidi na kupanda kwa gharama ya maisha, bei ya mafuta na malalamiko kuhusu hali ya uchumi.
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa jumla ya maandamano 1,292 yalirekodiwa nchini kati ya Januari 2025 na Juni 2026, huku mwaka 2025 ukishuhudia maandamano 839.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































