SERIKALI YAPENDEKEZA MIKOPO BADALA YA UFADHILI WA VYUO
Serikali imependekeza kufutwa kwa ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu na badala yake wanafunzi wote watakaojiunga na vyuo vikuu vya umma wapatiwe mikopo ya kugharimia asilimia 100 ya masomo yao, ambayo itarejeshwa baada ya kupata ajira.
Pendekezo hilo limo katika Mswada wa Ufadhili wa Elimu ya Juu unaolenga kuunganisha mfumo wote wa ufadhili wa elimu ya juu chini ya mamlaka moja itakayokuwa na jukumu la kusimamia fedha hizo.
Iwapo utapitishwa, mfumo huo utachukua nafasi ya utaratibu wa sasa ambapo baadhi ya wanafunzi hupata ufadhili wa masomo na wengine hupokea mchanganyiko wa ufadhili na mikopo kulingana na mahitaji yao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































