#Football #Sports

KAKAMEGA HIGH YATWAA TAJI LA KSSSA KWA MARA YA 13

Kakamega High almaaru The Green Commandoes  wametwaa ubingwa wa soka wa shule za upili baada ya kuwachapa St. Mary’s Yala mabao 3-2 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa M-Pesa Foundation Academy mjini Thika.

Ushindi huo umehitimisha ukame wa miaka saba kwa Kakamega High na kuifanya kutwaa ubingwa wa taifa kwa mara ya 13, idadi kubwa zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Kakamega High ilianza vyema kwa bao la mapema la Eugene Mbeleti, huku Yala ikifanya mashambulizi ya mwisho kusaka sare, lakini mabingwa hao walidumisha ushindi hadi filimbi ya mwisho na kurejesha taji lao la kitaifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *