#Football #Sports

GOR MAHIA YATINGA FAINALI CECAFA

Gor Mahia imefuzu kwa fainali ya Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA baada ya kuiondoa Al-Hilal Omdurman ya Sudan kwa mikwaju ya penalti 8-7 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mjini Kigali.

Mabingwa hao wa Kenya walitangulia kupata bao katika dakika ya 38, lakini Al-Hilal wakasawazisha dakika tano baadaye na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Baada ya sare hiyo kudumu hadi mwisho wa mchezo, Gor Mahia ilishinda kwa mikwaju ya penalti na sasa itachuana na Rayon Sport ya Rwanda katika fainali baada ya timu hiyo kuishinda Jamus ya Sudan Kusini mabao 3-1.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

GOR MAHIA YATINGA FAINALI CECAFA

KCB YAJIPANGA KABEBERI SEVENS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *