#Athletics #Sports

KENYA INAWANIA KUANDAA MASHINDANO YA DUNIA YA RIADHA 2029

Kenya imeingia rasmi katika kinyang’anyiro cha kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha 2029, baada ya Nairobi kuwasilisha ombi la kuandaa mashindano hayo makubwa ya kimataifa.

Nairobi sasa inachuana na London, Rome na Munich, ambazo pia zimewasilisha zabuni za kuandaa mashindano hayo huku Ombi la Kenya likiungwa mkono na serikali katika juhudi za kuleta mashindano hayo barani Afrika.

Iwapo Nairobi itafanikiwa, itakuwa mji wa kwanza barani Afrika kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya ngazi ya wakubwa, hatua ambayo itaweka Kenya katika historia ya riadha duniani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KENYA INAWANIA KUANDAA MASHINDANO YA DUNIA YA RIADHA 2029

LIGI KUU YA FKF KUANZA AGOSTI 29

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *