KAKAMEGA HIGH WAENDELEZA UBABE MICHEZO YA KSSSA
Mashindano ya Kitaifa ya Muhula wa Pili Shule ya Upili yanaendelea katika Chuo cha M-Pesa Foundation Academy huku timu mbalimbali zikipigania alama muhimu katika hatua ya makundi.
Katika soka la wavulana, mabingwa wa Mkoa wa Magharibi Kakamega High waliichapa Tumaini Boys mabao 4-0 huku Julius Ochieng akiifungia Kakamega bao la kwanza kabla ya Macline Adika, Daniel Ombati na Bradley Mulamba kuongeza mengine matatu na kuendeleza harakati za kutwaa ubingwa wa kitaifa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2018.
Katika mchezo mwingine wa wavulana, Menengai High waliwashangaza mabingwa watetezi Highway kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0, matokeo yaliyofanya ushindani katika kundi hilo kuwa mkali kuelekea michezo iliyosalia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































