#Local News

SHA BADO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NCHINI ASEMA MERCY MWANGANGI

Afisa Mkuu wa Mamlaka ya Bima ya Afya ya Jamii, SHA, Dkt. Mercy Mwangangi, amekiri kuwa bima hiyo   bado inakabiliwa na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya mfumo wa utoaji huduma za bima ya afya pamoja na ulaghai.

Kwa mujibu wa afisa huyo Changamoto hizo zinasababisha matatizo katika utoaji wa huduma kwa zaidi ya watu milioni 32 waliosajiliwa katika mpango huo kufikia sasa.

Huku haya yakijiri Waziri wa Afya, Aden Duale, amesema zaidi ya shilingi bilioni 164 zimelipwa kwa hospitali mbalimbali kwa huduma zinazotolewa chini ya SHA, huku kiasi cha shilingi bilioni 203 kikiwa kimekusanywa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

SHA BADO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NCHINI ASEMA MERCY MWANGANGI

LEE  KINYANJUI AWASUTA VIONGOZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *