#Football #Sports

RWANDA YANYAKUA UWENYEJI WA KAGAME CUP KWA MIAKA MIWILI

Rwanda imepewa haki ya kuandaa mashindano ya CECAFA Kagame Cup kwa misimu miwili ijayo, baada ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuidhinisha ombi hilo.

Rwanda itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwaka 2027 na 2028, kufuatia mafanikio yake katika kuandaa toleo la mwaka 2026.

Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha kamati kuu ya CECAFA kilichofanyika Agosti 6, huku Shirikisho la Soka Rwanda likiomba kuendeleza uenyeji wa mashindano hayo baada ya toleo la mwaka huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *