#Local News

MZOZO WA KIFAMILIA WAGEUKA MAUAJI NAKURU

Kinachoanza kama mzozo wa kifamilia wakati mwingine huishia katika matokeo ya kusikitisha, huku visa vya mauaji ya wanandoa vikiendelea kuzua wasiwasi nchini.

Polisi wamemkamata Caroline Chebet, mwenye umri wa miaka 37, kwa tuhuma za kumuua mumewe Alphonse Ochieng kwa kumchoma kisu nyumbani kwao katika eneo la Rongai, Kaunti ya Nakuru.

Majirani wamesema wanandoa hao walikuwa na migogoro ya mara kwa mara, huku mshukiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *