#Local News

OBURU OGINGA ASEMA KENYA INA UWEZO WA KUFIKIA SINGAPORE

Kiongozi wa ODM Oburu Odinga amesema Kenya inaweza kufikia kiwango cha maendeleo cha Singapore iwapo itatekeleza mikakati iliyosaidia taifa hilo kufanikiwa kiuchumi na kijamii.

Oburu amesema hatua ya kwanza ni kukabiliana na ufisadi kwa kujenga jamii ambayo haitavumilia vitendo vya ufisadi, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma.

Kiongozi huyo aidha  ameitaka serikali kuepuka ubadhirifu wa fedha za umma, akisema kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali katika maendeleo kutaiwezesha Kenya kufikia viwango vya juu vya maendeleo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *