#Local News

ICHUNG’WAH: HATUNA WASIWASI NA WANAOHAMA UDA

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah amesema chama cha UDA hakina wasiwasi kuhusu wanachama wanaohamia DCP.

Ichung’wah amesema serikali ya ushirikiano mpana ina muungano imara na iko tayari kukabiliana na changamoto za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Amesema wana imani kubwa kuwa muungano huo utashinda uchaguzi wa 2027, licha ya baadhi ya wanasiasa kuhama UDA na kujiunga na DCP.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *