#Business

KENYA KUUANDAA BAJETI YA KWANZA YA SH. TRILIONI 5.3

Serikali kuu inaandaa bajeti yake kubwa zaidi ya kitaifa kuwahi kutokea, huku matumizi ya mwaka wa fedha wa 2027/28 yakitarajiwa kuvuka kiwango cha Shilingi trilioni 5 kwa mara ya kwanza, wakati  serikali inalenga kupunguza nakisi ya bajeti.

Hazina ya kitaifa chini ya uongozi wake Waziri John Mbadi imependekeza bajeti ya Shilingi trilioni 5.323 kwa mwaka wa fedha wa 2027/28, kulingana na Rasimu ya Waraka wa Mapitio na Mtazamo wa Bajeti ambayo imetolewa mwezi huu. Bajeti hii inakuja wakati serikali ikiendelea na mpango wake wa kuimarisha hali ya fedha na kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Hazina inakadiria kuwa nakisi ya bajeti ya Kenya itakuwa Shilingi trilioni 1.321, sawa na asilimia 5.7 ya Pato la Taifa (GDP), ikiwa ni pungufu kutoka asilimia 6.2 katika mwaka wa fedha wa 2026/27. Ingawa nakisi hiyo inatarajiwa kupungua, serikali bado italazimika kukopa kiasi kikubwa cha fedha ili kuziba pengo kati ya mapato na matumizi.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *