ODM YAMSUTA GACHAGUA KWA KAULI KUHUSU KIFO CHA RAILA
Chama cha ODM kimemkosoa vikali kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kuhusu kauli zake zinazotia shaka mazingira ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na mwanzilishi wa chama hicho, Raila Odinga.
Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga amesema madai ya Gachagua kuhusu uwezekano wa mchezo mchafu katika kifo cha Raila hayana msingi na yanaweza kuongeza mgawanyiko nchini, wakati familia yake bado inaomboleza.
Wanga pia amekanusha uwezekano wa ODM kushirikiana na Gachagua, akimtuhumu kiongozi huyo wa DCP kuendeleza siasa za kikabila na zinazogawanya Wakenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































