#Local News

NYAMORI AMSUTA GACHAGUA KWA KAULI ZAKE DHIDI YA RUTO

Wakili wa Mahakama Kuu Joshua Nyamori amemkosoa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa madai yake kuhusu utendakazi wa serikali ya Rais William Ruto.

Nyamori amesema baadhi ya kauli za Gachagua kuhusu serikali ni uvumi, akidai kuwa hazina msingi wa kutosha na zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari.

Amesema Gachagua alitumia miaka miwili kati ya minne akiwa serikalini kama Naibu Rais, na kuhoji kwa nini hakuzungumzia changamoto hizo wakati huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *