#Local News

DEREVA WA MATATU ASAKWA KWA KUMDUNGA MSICHANA NA KUMTUPA PORINI

Polisi katika Kaunti ya Vihiga wanamsaka dereva wa matatu ya abiria 14 anayetuhumiwa kumdunga kisu msichana mwenye umri wa miaka 19 na kumtupa kwenye kichaka katika kaunti ya Vihiga eneo la Mbale.

Sylvia Moraa alikuwa amepanda matatu hiyo Agosti 3 akielekea Busia, lakini anasema alijikuta akielekea Kakamega kabla ya safari hiyo kugeuka kuwa ya hatari.

Dereva huyo anadaiwa kumdunga Sylvia na kumwacha akipigania maisha yake, huku mshukiwa akiendelea kusakwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *