ULINZI STARS YAWEKA MPANGO MPYA BAADA YA KUNUSURIKA KUSHUKA DARAJA
Ulinzi Stars imeanza maandalizi kwa nguvu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu baada ya kunusurika kushuka daraja msimu uliopita, huku kocha wa muda Mulinge Ndeto akilenga kujenga kikosi imara zaidi.
Ulinzi ilinusurika siku ya mwisho baada ya kuifunga Posta Rangers 1-0, katika msimu uliokuwa na mabadiliko ya makocha, matokeo yasiyoridhisha na ukosefu wa makali ya kufunga mabao.
Kikosi hicho kimeongeza kasi ya maandalizi ya msimu mpya, huku sehemu ya mazoezi ikihamishiwa eneo la Kibra Nairobi, ambapo benchi la ufundi linaangazia utimamu wa mwili, mbinu za mchezo na kujenga mshikamano wa kikosi kipya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































