MENENGAI OILERS YALENGA KULIPA KISASI KABEBERI SEVENS
Kocha wa Menengai Oilers Geoffrey Ominde amesema timu yake imefanyia kazi udhaifu wa kupokea mipira ya kuanza mchezo na nidhamu, ikilenga kutwaa ubingwa wa Kabeberi Sevens wikendi hii.
Oilers ilimaliza ya pili katika Dala Sevens baada ya kufungwa 17-5 na Kabras katika fainali, huku Ominde akisema wiki mbili zilizopita zimetumika kurekebisha makosa yaliyoigharimu timu hiyo ubingwa.
Ominde pia amewataka wachezaji wake kuwa na nidhamu na kuepuka adhabu za waamuzi, akisema kucheza na wachezaji sita dhidi ya Kabras kulichangia kushindwa kwao katika fainali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































