#Local News

VIONGOZI WA ODM WAUNGA MKONO AJENDA YA BEYOND VISION 2030

Msimamo kuhusu ajenda mpya ya maendeleo ya taifa unaendelea kujitokeza kutoka kwa viongozi wa kisiasa, huku baadhi ya vyama vikieleza kuunga kwa mkakati huo wa baada ya Dira ya 2030.

Viongozi wa ODM wakiongozwa na Oburu Odinga wameunga mkono ajenda ya Beyond Vision 2030, wakisema itasaidia kuimarisha maendeleo na usawa nchini.

Viongozi hao wamesema wanaunga mkono ajenda hiyo kwa kuwa chama hicho kilishiriki katika kuasisi Dira ya 2030, huku wakiwakosoa viongozi wa upinzani kwa kile wanachodai ni siasa zisizo na dira ya maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *