WAHUSIKA WA MAUAJI YA ALIYEKUWA MBUNGE GEORGE THUO KUHUKUMIWA LEO
Watu sita waliopatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa Mbunge wa Juja George Thuo watahukumiwa hii leo.
Sita hao Paul Wainaina Boiyo almaarufu Sheki, Christopher Lumbazio Andika maarufu Lumba, Andrew Karanja Wainaina, Samuel Kuria Ngungi almaarufu Visi, Esther Ndinda Mulinge, na Ruth Watahi Irungu almaarufu Atlanta.
Mahakama kuu ya Milimani mnamo Aprili mwaka huu ilitoa uamuzi kwamba sita hao walimpa sumu kwa pamoja Thuo eneo moja la burudani katika Kaunti ya Kiambu mnamo 2013 kwa kuweka kinywaji chake dawa ya kuua wadudu ya cyhalothrine.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 






























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































