MCK YAZINDUA MWONGOZO MPYA KWA WANAHABARI
Baraza la Wanahabari nchini MCK limezindua rasmi mwongozo mpya wa kuwaongoza wanahabari katika kuripoti uchaguzi mkuu ujao, huku hafla hiyo ikiendelea katika Kaunti ya Nakuru.
Mwongozo huo unalenga kuwapa wanahabari mbinu bora za kuripoti uchaguzi kwa uwajibikaji na kwa kuzingatia weledi, huku ukisisitiza umuhimu wa usahihi na usawa katika utoaji wa habari kwa umma.
Uzinduzi huo unafanyika wakati ambapo visa vya wanahabari kushambuliwa, kutishiwa na kuzuiwa kutekeleza majukumu yao vimeongezeka katika maeneo mbalimbali nchini, hali inayozua wasiwasi kuhusu usalama na uhuru wa wanahabari kuelekea uchaguzi mkuu.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































