SERIKALI YATAKIWA KUAGIZA CHAKULA KUTOKA NJE ASEMA KAGWE
Huenda serikali ikalazimika kuagiza baadhi ya vyakula kutoka nje ya nchi ili kuhakikisha Wakenya wanapata chakula cha kutosha, hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kaunti ya Trans Nzoia kutathmini athari za kiangazi, Kagwe amesema mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri pakubwa uzalishaji wa chakula nchini, hali ambayo huenda ikasababisha upungufu wa baadhi ya bidhaa muhimu za chakula.
Kagwe amesema hatua ya kuagiza vyakula kutoka nje inaweza kusaidia kuziba pengo la uzalishaji wa ndani na kuhakikisha mahitaji ya chakula nchini yanakidhiwa licha ya changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































