DIG LANGAT KIKAANGONI
Familia ya mwanablogu Albert Ojwang aliyefariki mikononi ma maafisa wa polisi baada ya kukamatwa imeendelea kudai haki ya mwanao, ikiwalaumu polisi kutokana na kifo hicho.
Ikiongozwa na Meshack Ojwang ambaye ni babake kijana huyo, familia hiyo imetilia shaka uwazi kwenye uchunguzi wa kifo hicho, kauli sawa ikishikiliwa na wanaharakati wanaoshinikiza kujiuzulu kwa naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Langat.
Aidha, wanaharakati hao wamemtaka Langat ambaye ndicho chanzo cha kukamatwa kwa Ojwang, ajiondoe kwenye uchunguzi unaoendelea.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































