ODM: ENZI BABA KWA KUTEKELEZA AJENDA ZAKE
Viongozi wa chama cha ODM wamemtaka Rais William Ruto kutekeleza ajenda 10 zilizo kwenye mktaba wa maelewano uliotiwa Saini na Rais na aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga, wakisema ndiyo njia mwafaka ya kumuenzi Odinga.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, naibu mwenyekiti wa ODM Godfrey Osotsi, amesema ajenda hizo zinawakilisha maslahi ya mwananchi wa kawaida, ambaye alitetewa na Odinga kila mara.
Miongoni mwa ajenda hizo ni fidia kwa waathiriwa wa dhuluma za polisi wakati wa maandamano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































