AMISI ADAI RUTO ALINUNUA ODM
Mbunge wa Saboti kaunti ya Trans Nzoia, Caleb Amisi, amehusisha masaibu ya chama cha ODM na mwingilio kutoka nje ya chama, akiibua madai kwamba Rais William Ruto amekinunua chama hicho huku wanachama chipukizi wakikabiliwa na vitisho vya kufurushwa.
Akizungumza wakati wa zoezi la kuwapokeza wanafunzi hundi za basari katika eneo la Matisi, Amisi amesema waliolengwa ni pamoja na mwanawe kinara mwanzilishi wa chama hicho Raila Odinga, Winnie Odinga, seneta Edwin Sifuna na mbunge Babu Owino.
Amekariri kuwa viongozi hao hawatayumbishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































