WATOTO, 15, UFARANSA WAZUIWA MITANDAONI
Wabunge nchini Ufaransa wamepitisha mswada ambao huenda ukapiga marufuku Watoto walio chini ya umri wa miaka 15 kutumia mitandao ya kijamii, hatua ambayo imeungwa mkono pakubwa na Rais Emmanuel Macron kama njia ya kuwalinda Watoto dhidi ya matumizi kupita kiasi ya sim una vifaa nyingine vya kielektroniki.
Mswada huo ulipitishwa na bunge la kitaifa ambalo ni la chini, na utwasilishwa katika bunge la seneti kabla ya kuwa sheria.
Kwenye mtandao wa kijamii wa X, Rais Macron ametaja uamuzi huo kuwa katua kubwa katika kuwalinda Watoto wa Ufaransa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































