VIONGOZI WA KENYA KWANZA KIPSIGIS WAMKOSOA GACHAGUA
Viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza kutoka jamii ya Kipsigis wamemkashifu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa matamshi yake kuwa jamii ya Kalenjin haina kiongozi anayezungumza kwa niaba yake.
Viongozi hao wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika bunge Seneti, Aaron Cheruiyot, wamesema kauli za Gachagua hazina msingi na zinalenga kuleta ubabe wa kisiasa ndani ya jamii hiyo.
Aidha wamesema jamii ya Kalenjin ina viongozi wake halali na kwamba si sahihi kwa mtu yeyote kudai kuwa hakuna uongozi unaowakilisha maslahi yao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































