#Football #Sports

UEFA: TIMU ZA EPL ZATAMALAKI RAUNDI YA 16

Klabu 6 zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, ni miongoni mwa timu 16 zinazosubiri kufahamu wapinzani wao kwenye raundi 16 katika dimba la klabu bingwa bara Ulaya hii leo.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu 6 kutoka EPL kufuzu raundi ya 16 ya dimba hilo.

Klabu hizo ni Arsenal walioshinda mechi zote za awamu ya makundi, Liverpool, Manchester City, Chelsea, Tottenham, na Newcastle waliofuzu kupitia mchujo wa mwondoano.

Klabu hizo zinajiunga na Bayern Munich, Barcelona, Sporting CP, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Atletico Madrid, Galatasaray, Bodo/Glimt, Atalanta na bingwa mtetezi, PSG.

Droo ya leo itatoa mwelekeo si tu kwa raundi ya 16, bali ramani kamili ya kuelekea robo fainali, semi fainali na baadaye fainali itakayoandaliwa jijini Budapest nchini Hungary.

Kama ilivyofanyika katika droo ya mwondoano, kila timu inaweza tu kukutana na moja kati ya timu mbili ambazo tayari zimejulikana.

Mfano, Real Madrid watachuana na Manchester City au Sporting CP, PSG wakabiliane na Barca au Chelsea huku Galatasaray wakiwa na uwezekano wa kukutanishwa na Liverpool au Tottenham.

Aidha, Atalanta watakutanishwa na mpinzani mmoja kati ya FC Bayern na Arsenal, nao Newcastle wakitarajia kumenyana na Chelsea au Barca.

Atletico Madrid watacheza na Liverpool au Tottenham, Bayer Leverkusen wacheze na Bayern au Arsenal

Iwapo Real Madrid watakutanishwa na Sporting, basi Man City watalazimika kukutana tena na Bodo Glimt, timu ya Norway ambayo imefahamika kuwaanguasha miamba msimu huu, waathiriwa wakiwa City wenyewe, Chelsea, Atletico na Inter Milan.

Mkondo wa kwanza wa raundi ya 16 utachezwa tarehe 10 na 11 mwezi ujao, na marudiano wiki moja baadaye.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UEFA: TIMU ZA EPL ZATAMALAKI RAUNDI YA 16

WELTEJI APIGWA MARUFUKU YA MIAKA 2

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *