JAJI WARSAME AAPISHWA RASMI
Jaji Mohamed Warsame ameapishwa rasmi hii leo kuwa jaji mkuu wa mahakama ya upeo nchini katika hafla iliyofanyika kwenye ikulu ya Nairobi,
Warsame anakua jaji wa kumi na nne wa mahakama ya juu zaidi nchini baada ya kujaza nafasi ilyowachwa wazi na jaji Mohamed Ibrahim aliyeaga dunia Decemba mwaka jana.
Rais William Ruto alimteua rasmi jaji huyo kupitia notisi kwa gazeti la serikali lililochapishwa tarehe 5 mwezi Mei mwaka huu.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































