#Rugby #Sports

KABRAS SUGAR WATWAA UBINGWA WA DALA 7S

Kabras Sugar RFC wametawazwa mabingwa wa Dala 7s baada ya kuichapa Menengai Oilers kwa alama 17-5 katika fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Kisumu.

Menengai Oilers walitangulia kufunga kupitia John Okoth kabla ya mapumziko, lakini Kabras walirejea kwa nguvu kipindi cha pili ambapo Rayvon Ambale alisawazisha alama baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jackson Siketa na kuiongoza timu yake kutwaa ubingwa.

Katika fainali ya wanawake, Mwamba RFC waliwashinda Kenya Harlequin kwa alama 12-7 huku Duru inayofuata ya Mzunguko wa Kitaifa wa Raga ya Wachezaji Saba ikifanyika Agosti 15 na 16 katika mashindano ya Kabeberi 7s jijini Nairobi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *