#Local News

RUTHU KULUNDU ATEULIWA KAMA KAIMU KATIBU WA IEBC

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC imemteua Ruth Kulundu kuwa Kaimu Katibu wa Tume na Afisa Mkuu Mtendaji.

Uteuzi huo unaanza kutekelezwa leo, Agosti 5, 2026, baada ya kumalizika kwa muda wa miezi sita wa Moses Ledama Sunkuli aliyekuwa akikaimu wadhifa huo.

Mwenye kiti wa IEBC Erustus Ethekon amesema Kulundu ataendelea kuwa kaimu katibu wa tume hiyo hadi mchakato wa kuajiri na kumteua Katibu wa Tume na Afisa Mkuu Mtendaji wa kudumu utakapokamilika.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *