MASENETA WAKOSOA KAUNTI KWA MATUMIZI HAFIFU YA FEDHA ZA MAENDELEO
Seneti imekosoa baadhi ya serikali za kaunti kwa kushindwa kutenga fedha za kutosha kwa miradi ya maendeleo, ikisema hali hiyo inakwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ripoti ya Utendaji wa Kifedha wa Kaunti ya mwaka wa fedha 2024/2025 imeonyesha kuwa kaunti 27 hazikufikia kiwango kinachopendekezwa cha matumizi ya maendeleo, huku Spika wa Seneti Amason Kingi akizishutumu kwa kuipa kipaumbele matumizi ya kawaida badala ya miradi ya maendeleo.
Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa matumizi ya maendeleo, ikifuatiwa na Turkana, huku Mandera, Kwale, Narok, Kiambu, Nakuru, Kitui na Wajir pia zikiorodheshwa miongoni mwa kaunti zilizofanya vizuri katika uwekezaji wa miradi ya maendeleo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































