#Local News

KUPPET YATOA NOTISI YA MGOMO KWA TSC

Shughuli za masomo zinaweza kutatizika mwishoni mwa mwezi huu baada ya walimu kutoa onyo la kuchukua hatua za viwandani kutokana na kucheleweshwa kwa kupandishwa vyeo.

Muungano wa Walimu wa Shule za Upili (KUPPET) kimeipa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) muda wa siku saba kuwapandisha vyeo walimu 16,000 waliosalia kati ya 50,000 walioahidiwa na Rais William Ruto.

KUPPET kinasema walimu 34,000 pekee ndio wamepandishwa vyeo hadi sasa, kikionya kuwa iwapo ahadi hiyo haitatekelezwa ndani ya muda uliowekwa, kitaanzisha mgomo wa kitaifa utakaovuruga muhula wa tatu wa masomo unaoanza mwishoni mwa Agosti.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *