#Sports #Volleyball

KESOGON NA CHESAMIS WATWAA UBINGWA WA TAIFA WA VOLIBOLI

Shule ya upili ya  Kesogon na Chesamis Boys wametwaa ubingwa wa taifa wa voliboli katika mashindano ya shule za upili yaliyofanyika mjini thika.

Kesogon ilitwaa taji la wasichana kwa mara ya tatu baada ya kuichapa Soweto Academy kwa seti 3-0 za 25-13, 25-10 na 25-18, na kuongeza ubingwa huo baada ya kutwaa mataji ya mwaka 2023 na 2026.

Kocha wa Kesogon John Marani amesema ushindi huo umetokana na mbinu bora za mchezo, huku akieleza kuwa sasa timu hiyo imeelekeza nguvu zake kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Shule za Afrika Mashariki (FEASSSA).

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *