UDA NA ODM WAKUTANA NAIVASHA KUJADILI MWELEKEO WA KISIASA
Viongozi wa vyama vya UDA na ODM wamekutana mjini Naivasha, Kaunti ya Nakuru, huku kukiwa na matarajio kuwa mpango wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 utajadiliwa.
Mkutano huo unafanyika wakati vyama hivyo vikiendelea kujenga uhusiano wa kisiasa.
Mkutano huo unatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa, ikiwemo ushirikiano kati ya UDA na ODM kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano huo katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































