KAUNTI 18 ZIPO HATARINI KUTOKANA NA EL NIÑO
Serikali imezitambua kaunti 18 zilizo katika hatari ya kukumbwa na athari za El Niño, huku ikiweka mikakati ya kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua nyingi.
Idara ya Hali ya Hewa imesema kuna uwezekano wa nchi kupata mvua nyingi kuliko kawaida kuanzia Oktoba mwaka huu,huku athari zake zikitarajiwa kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka ujao.
Nairobi, Mombasa na Kisumu zimetajwa kuwa miongoni mwa maeneo ya mijini yaliyo katika hatari kubwa, huku serikali ikiendelea kuandaa hatua za kukabiliana na mafuriko na athari nyingine zinazoweza kujitokeza.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































